Friday, March 17, 2017
Thursday, March 2, 2017
Ccm wamjibu haya Mjane wa Kapteni Komba kuhusu mafao ya mumewe
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimemtaka Mjane wa Marehemu, Kapteni Komba, Bi. Salome Komba kufuatilia malipo ya mafao ya mumewe kwa uongozi wa kundi la Tanzania One Theatre (TOT) ambako ndiko alikokuwa akifanyia kazi.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), Rodrick Mpogolo, ametoa maelekezo hayo ikiwa ni siku moja tu baada ya Salome kukaririwa akimuomba Mwenyekiti wa CCM, Rais John Magufuli aingilie kati kumsaidia ili alipwe mafao ya marehemu mume wake yanayofikia Shilingi Milioni 75.
Mpogolo amesema ofisi yao haiwezi kulizungumzia suala hilo kwa sababu masuala yanayohusu fedha yanapaswa kufafanuliwa vyema na uongozi wa kundi lao la TOT ambako Komba alikuwa akifanya kazi.
“Ofisi yao haiwezi kulizungumzia kwa sababu masuala yanayohusu fedha yanapaswa kufafanuliwa vyema na uongozi wa kundi lao la TOT ambako Komba alikuwa akifanya kazi,” amesema.
Kwa mujibu wa Bi. Salome, hadi sasa wakati mumewe akitimiza miaka miwili tangu afariki dunia, CCM imemlipa Shilingi Milioni 4.5 tu ikiwa ni sehemu ya malipo hayo huku akifuatilia kwa muda mrefu bila mafanikio kupata kiasi kilichobaki cha Shilingi milioni 70.5 bila mafanikio.
Komba aliyezaliwa mwaka 1954, alifariki dunia Februari 28, 2015 na kuzikwa Mkoani Ruvuma ambako enzi za uhai wake alijizolea umaarufu mkubwa kutokana na umahiri wake katika kutunga na kuimba nyimbo mbalimbali za kwaya, hasa za kukipigia debe chama chake (CCM) wakati wa kampeni mbalimbali za uchaguzi.
RAIS DKT. MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI KIWANDA CHA VIGAE CHA GOOD WILL (MKURANGA), PIA AHUTUBIA WANANCHI WA IKWIRIRI, SOMANGA NA NANGULUKULU NA MCHINGA MKONI LINDI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Balozi wa China hapa nchini Dkt. Lu You qing mara baada ya kuweka jiwe la Msingi katika Kiwanda kikubwa cha kutengeneza Vigae(Tiles ) cha Good Will kilichopo katika kijiji cha Mkiwa, Mkuranga mkoani Pwani. Kiwanda hicho kitakuwa na uwezo wa kuzalisha vigae laki nane kwa siku na mwekezaji ametumia zaidi ya Dola mil.50 katika uwekezaji huo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Balozi wa China hapa nchini Dkt. Lu You qing akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Kiwanda hicho cha vigae kilichopo Mkiwa Mkuranga mkoani Pwani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisisitiza jambo wakati akihutubia kabla ya kuweka jiwe la Msingi katika Kiwanda kikubwa cha kutengeneza Vigae(Tiles ) cha Good Will kilichopo katika kijiji cha Mkiwa, Mkuranga mkoani Pwani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi wa Ikwiriri mkoani Pwani wakati alipokuwa akielekea mkoani Lindi na Mtwara katika ziara yake ya kikazi ya siku nne.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisikiliza maelezo kutoka kwa Mwakilishi wa Kiwanda hicho cha y Vigae cha Good Will, Huang Heng Chao kutoka kwa Kiwandani hapo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa anapata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo kuhusu matumizi ya Gesi katika Kiwanda cha Vigae cha Good Will kutoka kwa Kiwandani hapo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi wa Somanga mkoani Lindi wakati akiwa ziarani lkuelekea mikoa ya Kusini(Lindi na Mtwara).
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Mbunge wa Kilwa Kusini Suleiman Bungara(Bwege ) kutoka CUF katika eneo la Somanga wakati alipokuwa akielekea Nangulukulu katika ziara yake ya mikoa ya Kusini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Mbunge wa Kilwa Kusini Suleiman Bungara(Bwege ) kutoka CUF katika eneo la Nangulukulu, Kilwa mkoani Lindi wakati akiwa katika ziara ya mikoa ya kusini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi wa Nangulukulu mkoani Lindi.
Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo Nape Nnauye akifurahia hotuba iliyokuwa ikitolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika eneo la Nangulukulu mkoani Lindi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo Nape Nnauye mara baada ya kuhutubia wananchi wa Nangulukulu mkoani Lindi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimian na mbunge wa Kilwa Kaskazini Vedasto Ngombale (CUF) mara baada ya kuhutubia wananchi wa Nangulukulu mkoani Lindi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na wananchi mara baada ya kuhutubia wananchi wa Nangulukulu mkoani Lindi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpatia msaada wa Shilingi milioni moja kijana Abdulrahman Khalid ambaye ni mlemavu wa miguu katika eneo la Mchinga-1 mkoani Lindi, Katikati(Mwenye shati la maua) ni Mbunge wa Mchinga Hamidu Bobali kupitia chama cha (CUF) ambaye ameahidi kumpatia mlemavu huyo kiasi cha Shilingi Milioni moja pia.
.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa kiwanda cha kutengeneza vigae (Tiles) cha Tanzania Goodwill Ceramic Tiles Ltd mara baada ya kuweka jiwe la msingi leo Wilayani Mkuranga, Pwani. Kiwanda hicho kitakuwa na uwezo wa kuzalisha tani 8000 za Vigae kwa siku.Kushoto kwake ni Balozi wa China nchini Tanznia Dkt.Lu Youqing na kulia kwake ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji Dkt. Adelhelm Meru na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika kiwanda cha kutengeneza vigae (Tiles) cha Tanzania Goodwill Ceramic Tiles Ltd leo Wilayani Mkuranga, Pwani. Kiwanda hicho kitakuwa na uwezo wa kuzalisha tani 8000 za Vigae kwa siku.Kushoto kwake ni Balozi wa China nchini Tanznia Dkt.Lu Youqing na kulia kwake ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji Dkt. Adelhelm Meru na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji Dkt. Adelhelm Meru (kulia) akimsikiliza kwa makini Naibu Mkurugenzi wa kiwanda cha kutengeneza vigae (Tiles) cha Tanzania Goodwill Ceramic Tiles Ltd, Robin Huang (kushoto) wakati wa hafla ya kuweka jiwe la msingi la kiwanda hicho leo Wilayani, Mkuranga.Katikati ni Mmoja wa wafanyakazi wa kiwanda hicho jina lake(limehifadhiwa).
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwaaga wananchi na wafanyakazi wa kiwanda cha kutengeneza vigae (Tiles) cha Tanzania Goodwill Ceramic Tiles Ltd kilichopo Mkuranga Mkoani Pwani mara baada ya kuweka jiwe la msingi leo wilayani Mkuranga, Pwani.
Baadhi ya wananchi wakitawanyika mara baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli (hayupo pichani) kuondoka baada ya kuweka jiwe la msingi la kiwanda cha kutengeneza vigae (Tiles) cha Tanzania Goodwill Ceramic Tiles Ltd kilichopo Mkuranga, Pwani.
MBOWE ANG’ANG’ANIWA TENA MAHAKAMANI
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) iliyodai kuwa imeshindwa kuwapata kwa kutumia hati za wito za Mahakama, Freeman Mbowe, mkewe Dk Lilian Mtei na aliyekuwa Meneja wa Klabu ya Bilicanas, Steven Mligo kujibu mashtaka yanayowakabili, jana ilisaidiwa namna ya kuwafikia watu hao.
Mahakama ya Wilaya ya Ilala, ilitoa barua ya wito wa kuwataka wahudhurie mahakamani Machi 21, baada ya kufikia uamuzi wa kutoa wito huo kupitia magazeti.
Mbowe ambaye ni Mbunge wa Hai na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni na mkewe, Dk Mtei ni wakurugenzi wa Kampuni ya Mbowe Hotels Ltd.
Wawili hao pamoja na Mligo, Katika kesi hiyo namba 402 ya mwaka 2016, wanakabiliwa na mashtaka matatu ya kushindwa kutumia mashine za kielektroniki (EFD) kutoa risiti kinyume na kifungu cha 86 cha Sheria ya Usimamizi wa Kodi ya mwaka 2015.
Mashtaka mengine ni kuipotosha mamlaka kwa kutoa nyaraka za uongo kinyume na kifungu cha 84 na kushindwa kutekeleza masharti ya Sheria ya Usimamizi wa Kodi kinyume na kifungu cha 82 cha sheria hiyo.
Wanadaiwa kutenda makosa hayo Mei, 2016 jijini Dar es Salaam.
Imedaiwa kuwa tangu kesi hiyo ilipofunguliwa mwishoni mwa mwaka jana, imeshatajwa mara nne bila washtakiwa kufika mahakamani.
Wakili wa TRA, Marcel Busegano aliieleza Mahakama kuwa wamejaribu kuwapelekea washtakiwa hati za wito wa kufika mahakamani mara nne lakini wameshindwa kuwapata.
Alidai Meneja wa TRA Mkoa wa Ilala alijaribu kumpigia simu ya mkononi Mbowe lakini hakumpata na, hata walipokwenda katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) anakofanya kazi mkewe, Dk Mtei pia hawakumpata.
Kutokana na hali hiyo, TRA iliiomba Mahakama iamuru watumie tangazo gazetini kuwaita washtakiwa mahakamani na iwapo korti itakubali ombi hilo, tangazo litolewe kabla ya tarehe nyingine ya kutajwa kwa kesi hiyo.
Shauri hilo linalosikilizwa na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Ritha Tarimo litatajwa Machi 21.
Kutokanana na ombi hilo, tangazo hilo linapaswa kutangazwa gazetini kabla ya tarehe hiyo.
Wednesday, March 1, 2017
Mshambuliaji wa DR Congo kutocheza kwa wiki sita
Mshambuliaji wa klabu ya Hull City Dieumerci Mbokani hatocheza kwa kipindi cha wiki sita baada ya kupata jeraha la paja.
Hull pia imethibitisha kuwa jeraha la goti alilopata beki Harry Maguire wakati wa mechi dhidi ya Burnley sio baya sana zaidi ya ilivyodhaniwa.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 huenda akapona tayari kwa safari ya kueleka Leicester City siku ya Jumamosi.
Subscribe to:
Comments (Atom)
























